FAO yataka kilimo kipatiwe kinga inayofaa katika nchi masikini

29 Aprili 2008

Jacques Diouf, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) amewasilisha ripoti muhimu iliopendekeza jumuiya ya kimataifa kujinyakulia fursa iliojitokeza hivi sasa ili kurasimu mipango mipya ya kujikinga na tatizo la chakula, tatizo ambalo huenda likaibuka tena katika siku zijazo. Alitaka misaada ya wahisani wa kimataifa iwekezwe zaidi kwenye sekta ya kilimo.

Alisema bei ghali ya chakula inaweza kudhibitiwa na miradi ya aina mbili – awali, jumuiya ya kimataifa inatakiwa iandae mipango ya kuwasaidia mamilioni ya mafukara ambao mifumko ya kasi ya bei za chakula katika soko la kimataifa imeathiri sana njia zao za kujipatia riziki. Pili, Diouf amependekeza wakulima waliopo katika mataifa yanayoendelea wasaidiwe kuimarisha makulima yao kwa siku za usoni, kwa kuwapatia vifaa vinavyohitajika kuongeza uzalishaji, kwa kuwapatia ardhi zenye rutuba, uwezo wa kuyafikilia majkwa urahisi, na pia vitu vyenginwe vya lazima kama mbolea watakayoweza kuimudu pamoja na mbegu.

Mapendekezo ya Diouf yanaashiriwa, pindi yatatekelezwa, yatasaidia vilivyo umma wa vijijini kuzalisha mavuno kwa wingi, shughuli ambazo pia zitazalisha ajira ya mashambani itakayowasaidia wakazi wamaeneo hayo kujiendeleza kimaisha.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter