Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

CEB kuanzisha tume mpya kudhibiti mfumko wa bei za chakula duniani

CEB kuanzisha tume mpya kudhibiti mfumko wa bei za chakula duniani

Baada ya mashauriano siku mbili kwenye mji wa Bern, Uswiss baina ya KM Ban Ki-moon na viongozi wa lile bodi la wakurugenzi wa mashirika 27 ya UM (CEB), ambapo kulizingatiwa hatua za dharura za kukabiliana na mzozo wa kupanda kwa bei za chakula na nishati duniani, kuliafiwa na washiriki wa mashauriano hayo kuanzisha tume mpya maalumu ya kazi, itakayoshughulikia taratibu za kuudhibiti vyema mgogoro kwa kuwasaidia zaidi ule umma wa kimataifa ulio dhaifu.

Katika mkutano aliofanya kwenye mji wa Berne na waandishi habari Ijumanne, KM Ban aliihimiza jamii ya kimataifa kutekeleza ahadi za kusaidia taasisi za UM zinazohusika na huduma za kugawa chakula kwa umma muhitaji, na pia kuhakikisha kuna akiba ya kutosha ya chakula kukidhi mahitaji ya chakula wakati wa dharura.

Sikiliza ripoti kamili kwenye idhaa ya mtandao.