Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sahihisho kuhusu makala ya J. Holmes katika Al-Ahram

Sahihisho kuhusu makala ya J. Holmes katika Al-Ahram

Ripoti ya Ijumaa kuhusu makala ya John Holmes, Naibu KM anayehusika na Masuala ya Kiutu, iliochapishwa kwenye gazeti la kila siku la Misri la Al-Ahram ilikosea kuhusu siku ambayo ilichapishwa. Kwenye ripoti yetu tulisema makala ya Holmes ilichapishwa Alkhamisi, tarehe 06 Machi, taarifa ambayo haikuwa sahihi. Tarehe sawa ya kuchapishwa makala ya Holmes, ilikuwa Ijumanne, 04 Machi 2008, ambapo alichukua fursa ya kuihimiza jamii ya kimataifa kujizatiti na kutafuta suluhu ya dharura kipamoja ili kusuluhisha mzozo wa Mashariki ya Kati.~~