Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM inaunga mkono uamuzi wa Serikali ya Usomali kuwasiliana na upinzani

UM inaunga mkono uamuzi wa Serikali ya Usomali kuwasiliana na upinzani

Ofisi ya UM juu ya Masuala ya Siasa kwa Usomali (UNPOS)imeripoti kwamba Mjumbe Maalumu wa KM kwa Usomali, Ahmedou Ould-Abdallah amepongeza uamuzi wa Serikali ya Mpito (TFG) ya Usomali kwa kupendekeza kukutana na wawakilishi wa vyama vya upinzani, ili wazingatie kipamoja taratibu za kurudisha tena nchini mwao utulivu na amani. Kwa mujibu wa Ofisi ya UNPOS, makundi yote husika yameafikiana kwamba pindi mazungumzo ya amani yatafanyika yaongozwe na Mjumbe wa KM, Ould-Abdallah, ambaye sasa hivi anashughulika kuwasiliana nawo kutayarisha kipamoja tarehe na mahali pa kukutana kuendeleza majadiliano yao.