Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Amani katika Maziwa Makuu inatathminiwa na Baraza la Usalama

Amani katika Maziwa Makuu inatathminiwa na Baraza la Usalama

Baraza la Usalama linatazamiwa, katika Alkhamisi ya leo, kupiga kura azimio la kuyashurutisha makundi yote ya kigeni yenye silaha, na yanayoshiriki kwenye mapigano haramu katika JKK, kusalimisha, haraka iwezekanavyo, silaha zao kwa wenye madaraka nchini. Azimio hili la Baraza la Usalama liliodhaminiwa na Ufaransa, pia limetilia mkazo ya kuwa makundi haya ya wanamgambo wa kigeni wawaachie huru watoto wote waliowateka nyara na kuwalazimisha kushiriki kwenye vitendovyao haramu.~ ~