Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano na NKM juu ya hali katika Kenya

Mahojiano na NKM juu ya hali katika Kenya

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alipozuru Kenya karibuni alitoa mwito maalumu kwa raia wote wa Kenya kusitisha haraka vitendo vya utumiaji nguvu na vurugu lilioharibu taifa lao katika wiki za karibuni. Alitaka vitendo hivyo vikomeshwe kwa masilahi ya "umma wa Kenya na taifa la Kenya, halkadhalika;" hasa ilivyokuwa machafuko haya yalisababisha vifo vya watu 800 ziada, na pia robo milioni nyengine kunyimwa makazi. KM Ban alisisitiza UM upo tayari kuisaidia ile Tume ya Watu Mashuhuri wa Afrika, inayoongozwa na KM Mstaafu Kofi Annan, kusuluhisha kwa njia za amani mgogoro uliozuka nchini tangu mwezi uliopita, baada ya Raisi wa Kenya Mwai Kibaki alipotangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi mbele ya mgombania wa upinzani Raila Odinga. KM Ban aliwaambia viongozi wa Kenya kwamba Umoja wa Mataifa upo tayari kujumyuihs amchango wake kihali na mali ili kurudisha tena hali ya usalama na amani nchini mwao.

Sikiliza mahojiano kamili kwenye idhaa ya mtandao.