Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jimbo la mtafaruku Sudan Magharibi lachambuliwa kwa kina na Mjumbe Maalumu wa UA kwa Darfur

Jimbo la mtafaruku Sudan Magharibi lachambuliwa kwa kina na Mjumbe Maalumu wa UA kwa Darfur

Mnamo mwezi Juni wapatanishi bia wa Umoja wa Mataifa (UM) na Umoja wa Afrika (UA) - yaani Jan Eliasson na Salim Ahmed Salim, kwa kufuatana - waliwasilisha ripoti mbele ya wajumbe wa Baraza la Usalama kuhusu juhudi zao shirika za kusuluhisha mzozo wa kisiasa ulioyakabilia makundi husika na suala la Darfur, ikijumlisha Serikali ya Sudan, makundi ya waasi na wadau wengineo wa kitaifa na kimataifa. Eliasson na Salim walidhihirisha kuwa na mashaka kama makundi yanayohusika na mvutano wa Darfur kweli wapo tayari kushauriana au kusikilizana na kukubaliana kwa maridhiano kuwasilisha amani, na kukomesha mzozo katili wa miaka mitano uliolivaa eneo lao katika Sudan magharibi.~

Mtayarishaji vipindi wa Redio ya UM, A. Z. Rijal alipata fursa ya kufanya mahojiano makhsusi na Mjumbe Maalumu wa UA kwa Darfur, Salim Ahmed Salim ambaye alitupatia uchambuzi wa jumla, na wa kina kikuu, kuhusu suala la Darfur. Mahojiano haya yatawawezesha wasiklilizaji kuwa na ufahamivu mzuri zaidi wa kuelewa mchangamano au utata uliojiri kwenye juhudi za kutatua tatizo la Darfur katika siku za karibuni.

Sikiliza mahojiano kamili kwenye idhaa ya mtandao ya Redio ya UM.