Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na pale

Hapa na pale

Ofisi ya UM ya Kudhibiti Uhalifu na Madawa ya Kulevya (UNODC) iliopo Vienna, Austria imeandaa mkutano maalumu wa kuzingatia hatua za kuchukuliwa haraka kukomesha biashara haramu ya kunyakua watu ambao baadaye hulazimishwa kushiriki kwenye ajira za umalaya na vibarua vyengine nje ya sheria; kikao ambacho kilijumuisha watu 1,200 wakiwemo wataalamu, wabunge, watumishi wa usalama, viongozi wa biashara na wawakilishi wa mashirika yasio ya kiserekali na pia waathiriwa wa biashara ya utumwa mambo leo kutoka mataifa 116.~

Ray Chambers, raia wa Marekani ameteuliwa na KM Ban Ki-mmon kuwa Mjumbe wake Maalumu Kuhusu Masuala ya Malaria.

Shirika la UM juu ya Udhibiti wa Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) limetoa ombi linalopendekeza lifadhiliwe dola milioni 500 zitakazotumiwa kupunguza vifo vya mama wajawazito na kukomesha matatizo ya uzazi kwenye mataifa 75 duniani.

Mkutano wa siku tatu wa Baraza Kuu la UM kuhusu athari za mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni umemalizika baada ya wajumbe 115 kubashiria hatari iliokabili mazingira na umma wa kimataifa hivi sasa pindi matatizo hayo hayajadhibitiwa, masuala ambayo Raisi wa Baraza Kuu Srgjan Kerim alisema yanahitajia ushirikiano wa pamoja kuyasuluhisha kidharura kwa ridhaa ya jamii yote ya kimataifa.