28 Februari 2008
Askari wa Polisi kutoka Bangladesh wanaowakilisha Vikosi Mseto vya UM/UA kwa Darfur (UNAMID) vimeanzisha doria ya majaribio, za masafa marefu ya kilomita 200, zilizoanzia kwenye kambi zao katika mji wa Nyala, Darfur Kusini na kuendelea hadi mji mkuu wa Darfur Kaskazini wa El-Fasher.