Skip to main content

KM wa UM ayapongeza maafikiano ya Serikali ya Muungano Kenya

KM wa UM ayapongeza maafikiano ya Serikali ya Muungano Kenya

KM Ban Ki-moon ameyapongeza, kwa moyo thabiti, yale “Maafikiano ya Ushirikiano wa Serikali ya Muungano” kwa Kenya, yaliyotangazwa Alkhamisi mjini Nairobi ambapo juhudi za kusuluhisha kipamoja mzozo uliolivaa taifa baada ya matokeo ya uchaguzi, zimezalisha mafanikio ya kuridhisha.

KM Ban alizisifu juhudi za Raisi Mwai Kibaki na Raila Odinga (wa ODM) pamoja na mchango wao wa maelewano na masikilizano yaliosaidia pakubwa kukamilisha mapatano yao chini ya uongozi wa KM Mstaafu Kofi Annan.

Tutakuwa na ripoti ziada juu ya mwafaka huo kwenye taarifa ya habari za Ijumaa.