Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya UM zapungua 2007 Liberia

Tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya UM zapungua 2007 Liberia

Ripoti ya karibuni ya Shirika la UM juu ya ulinzi wa amani katika Liberia (UNMIL) imethibitisha kwamba shtumu dhidi ya wafanyakazi wa UM, ambao siku za nyuma walidaiwa kuendeleza ukandamizaji na tuhumu za unyanyasaji wa kijinsia, zimeteremka kwa asilimia 80 katika kipindi cha nusu ya pili ya mwaka 2007, tukilinganisha na kipindi hicho hicho katika 2006.

Licha ya mafanikio haya UNMIL imeripoti kwamba haitoruhusu kamwe wala kustahamili abadan vitendo vyote vinavyohusikana na udhalilishaji wa kijinsia kwenye maeneo ya operesheni za amani katika Liberia.