Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwendesha Mashitaka Mkuu wa ICC azuru JAK

Mwendesha Mashitaka Mkuu wa ICC azuru JAK

Luis Moreno-Ocampo, Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya Kimatifa juu ya Jinai ya Halaiki (ICC) ameelekea Jamhuri ya Afrika ya Kati wiki hii kukutana na waathiriwa wa makosa karaha ya jinai ya vita yalioendelezwa nchini katika kipindi cha baina ya miaka ya 2002 na 2003. Kadhalika, atakapokuwepo mjini Bangui, JAK Moreno-Ocampo atakutana, kwa mashauriano, na wawakilishi wa jumuiya za kiraia, wenyeji husika na watumishi wa serikali. Ziara hii inafuatia tangazo la mwezi Mei 2007 ambapo Mwendesha Mashitaka aliripoti kwamba ataanzisha uchunguzi maalumu kuambatana madai ya kuwa jinai ya vita iliendelezwa dhidi ya utu, hususan yale makosa yanayoambatana na udhalilishaji wa kijinsia. Uchunguzi unafanyika kufuatia ombi liliopokewa na Mahakama kutoka Serikali ya JAK.

Ofisi ya ICC iliopo JAK vile vile inafanya uchunguzi kuhusu vitendo vya utumiaji mabavu vilivyofanyika katika sehemu za kaskazini tangu 2005.