Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti ya KM yasema "unyong'onyevu" wa maisha umetandaa Guinea-Bissau

Ripoti ya KM yasema "unyong'onyevu" wa maisha umetandaa Guinea-Bissau

Katika ripoti ya karibuni ya KM juu ya Guinea-Bissau ilibainishwa kwamba katika miezi michache iliopita imeonesha kuwepo muongezeko wa hisia za mzoroto wa maendeleo ya jamii nchini, mwelekeo ambao uliharibiwa zaidi na imani ya raia kwamba taasisi za kuendesha shughuli za taifa hazina dira ya mwongozo na zinaelea huku na huko dhidi ya maslahi ya umma.

Hata hivyo, ripoti ilisema KM amefurahika na hatua zilizochukuliwa karibuni na Serikali katika maandalizi ya uchaguzi wa bunge; na amependekeza ile Ofisi ya Kusaidia Ujenzi wa Amani katika Guinea-Bissau iongezewe muda wa kazi nchini hadi mwisho wa Disemba 2008 kuimarisha utulivu na kufufua kadhia za kiuchumi na jamii.