Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na pale

Hapa na pale

Kikundi Kazi cha Baraza Kuu kinachosimamia juhudi za kukomesha na kufyeka ukandamizaji wa kijinsia, na unyayanyasaji miongoni mwa watumishi wa UM, wamepitisha azimio muhimu karibuni litakalowahakikishia waathiriwa wa unyanyasaji wa kijinsia kuwa wanapatiwa tiba maridhawa, ushauri, misaada ya jamii na vile vile msaada wa kisheria.

Vikosi mseto vya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika (AU) juu ya ulinzi wa amani katika Darfur (UNAMID) vinatarajiwa kuanza rasmi operesheni zake Sudan tarehe 31 Disemba 2007, baada ya kukabidhiwa madaraka na vikosi vya AU vya AMIS, kwa kufuatana na mapendekezo ya azimio la Baraza la Usalama nambari 1769 la tarehe 31 Julai (2007).

Saad Houry, raia wa mataifa ya Lebanon/Kanada ameteuliwa na Katibu Mkuu Ban Ki-moon kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF).

Kuanzia tarehe mosi hadi mwisho wa Januari 2008 taifa la Libya litakabidhiwa uraisi wa duru wa Baraza la Usalama.

[na hatimaye] Mnamo tarehe 23 Disemba 2007, baada ya majadiliano makali kumalizika katika Baraza Kuu, kuzingatia bajeti la UM kwa 2008–2009, michuano ambayo ilishtadi hadi saa za usiku sana, wajumbe wa Mataifa Wanachama walifanikiwa kupitisha azimio la kuifadhilia Ofisi ya Shughuli za Utawala ya UM bajeti la dola bilioni 4.17; mataifa 141 yalipiga kura ya upendeleo na Marekani pekee ilitia kura ya upinzani; na azimio lilikhitimisha awamu ya kwanza ya kikao cha 62, cha mwaka huu cha Baraza Kuu.