Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM kutathminia uharibifu wa mazingira katika Ogoni, Nigeria

UM kutathminia uharibifu wa mazingira katika Ogoni, Nigeria

Shirika la UM juu ya Hifadhi ya Mazingira (UNEP) pamoja na Shirika la UM juu ya Miradi ya Maendeleo (UNDP) yamekamilisha, kwa kina, mjini Abuja, Nigeria na Serikali ya Nigeria maafikiano ya kuanzisha tathmini ya jumla kuhusu athari za mazingira zinazochochewa na shughuli za uchimbaji mafuta kwenye jimbo la Ogoni liliopo katika eneo la Nile Delta.

Muafaka huu ni mojawapo ya juhudi za Serikali ya Nigeria katika kurudisha tena utulivu na amani katika jimbo la Ogoni, baada ya mafuta kuanza kuchimbwa mnamo 1950, huduma iliyozusha vurugu la mara kwa mara kwenye eneo hilo.