Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa viongozi kuimarisha uwezo wa utekelezaji wa nchi za Kiafrika

Mkutano wa viongozi kuimarisha uwezo wa utekelezaji wa nchi za Kiafrika

Akifungua mkutano wa pili wa viongozi ulotayarishwa na taasisi ya kuimarisha uwezo wa utekelezaji barani Afrika, ACBF mjini Maputo Msumbiji, Rais Armando Guebuza wa Msumbiji, alisema suluhisho kwa matatizo ya Afrika yanabidi kutanzuliwa kwa kuendelea kuimarisha uwezo wa taasisi zake, kwa upande wa watumishi, fedha na mali.

Mkutano huo wa siku tatu ulohuduriwa na viongozi, wasomi, wanasiasa na wataalamu wa uchumi kutoka sehemu zote za Afrika, ulianza kwa arsha juu ya jinsi kuziwezesha nchi za Kiafrika kuongeza uwezo wa kazi na ujuzi wa wakazi wake kwa ajili ya maendeleo. Rais Guebuza mwenyeji wa mkutano alisema, inadbidi Waafrika wajiamini wenyewe na kubuni teknolojia zinazo lingana na mahitaji halisi ya Waafrika. Elizabeth Adhiambo Omolo, Mkurugenzi mkuu wa Shule ya taaluma ya Fedha ya Kenya alizungumza na Redio ya UM na alisema Rais Guebuza aligusia masuala mengi lakini alisisitiza kwamba:

Omolo....

Rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa, alihudhuria mkutano na alisema walitafakari na kubadilishana uzoefu wao chini ya misingi ifuatayo:

Mkapa.....

Tatizo moja kubwa lililojadiliwa ni kuondoka kwa wasomi na wataalumu wa Afrika kuelekea nje kutafuta maisha bora. Akizungumza suala hilo Bw. Mkapa alisema:

Mkapa....

Na wajumbe kwenye mkutano wanadhani ni viongozi wa nchi za Kiafrika wanaowajibika kuandaa mikakati kupunguza wimbi la watu kukimbia kutoka Afrika kuelekea nchi za n'gambo mara nyingi wakitumia njia za hatari. Bi Omolo anasema :

Omolo....

Nae naibu mkurugenza wa Ushirika Mpya kwa Ajili ya Maendeleo ya Afrika, NEPAD, Dk. Hesphina Rukato anasema:

Rukato:

Na kizingiti kingine kikuu cha maendeleo ya Afrika ni ulaji rushwa. Wajumbe kwenye mkutano huo wa Maputo wametoa mwito kwa serekali kuchukua hatua zaidi kupambana na janga hilo. Rais Mkapa alisema:

Mkapa....

Mkutano huo wa ACBF unaofanyika kila baada ya miaka mitano umegharimiwa na Benki Kuu ya Dunia na mashirika ya UM na wafadhili wa nchi za magharibi na kuhudhuriwa na wajumbe karibu 700. Maazimio kadhaa yalipitishwa na Dk. Rukato amesema:

Rukato....

Kuhusu mchango wa mashirika ya UM katka nyanja ya kuimarisha uwezo wa Afrika Dk. rukato alisema:

Rukato....

Kufikia malengo hayo kuna changa moto chungu nzima na Rais Guebuza wa Msumbiji alisema la muhimu ni kubadili mawazo na fikra za Waafrika ili kuweza kujiamini na kujitegemea wenyewe na kuacha kuwalaumu wageni, au kuwategemea zaidi. Nae Dk. Rukato anaunga mkono wazo hilo akisema:

Rukato....

Watayarishaji wa mkutano wa ACBF wameridhika na matokeo na hivi sasa la muhimu ni utekelezaji wa maazimio ili kuepukana na tabia ya wakuu kukutana bila ya kuwepo na ufwatiliaji wa maazimio.

Rukato....

Suala la ikiwa nchi za Kiafrika zitaweza kutekeleza Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) kufikia 2015 ili kupunguza umaskini kwa nusu limekua likitajwa katika majukwa mbali mbali. Na mkutano wa Maputo umezizitiza kwamba kuna haja kubwa ya kuimarisha uwezo wa nchi za Kiafrika katika nyanja zote kuweza kufikia malengo hayo.