Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tathmini ya Mradi wa Milenia, Mbola, Tanzania (Sehemu ya II)

Tathmini ya Mradi wa Milenia, Mbola, Tanzania (Sehemu ya II)

Katika makala iliopita tulikupatiani fafanuzi, za awali, za Dr. Gershon Isaac Nyadzi, mratibu wa sayansi na pia Mtafiti Mwandamizi anayeongoza timu ya wataalamu wanaohusika na utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia katika kijiji cha Mbola, katika mkoa wa Tabora, Tanzania. Alitupatia maelezo kuhusu namna vijiji vya majaribio, vilivyoanzishwa barani Afrika na UM, ikijumisha kijiji cha Sauri, kiliopo Kisumu, Kenya na pia Kijiji cha Mbola, katika Tanzania.

Madhumuni ya huduma hizo ilikuwa ni kuchunguza kama shughuli za maendeleo zinaweza kutekelezwa, na kuimarishwa, kwa kuanzia, awali, ngazi ya kijiji na hatimaye kuwapatia wakazi wa vijiji hivyo chakula, afya bora, elimu nzuri, usawa wa kijinsiya, utunzaji wa mazingira na pia utawala bora ambao ulidhamiriwa kuwahamasisha raia hao kuchangisha zaidi kwenye kadhia za kukuza maendeleo yao.

Makala ya sasa inakamilisha imazungumzo na Dr. Nyadzi pamoja na mfululizo wa vipindi vyetu juu ya mradi wa Maendeleo ya Milenia katika kijiji cha Mbola, kiliopo mkoani Taboraa, Tanzania.

Sikiliza ripoti kamili kwenye idhaa ya mtandao.