Upungufu wa fedha unahatarisha aila za Sahara Magharibi mipakani Algeria

7 Septemba 2007

UM imetangaza kuwepo upungufu wa asilimia 50 wa msaada wa fedha zinazohitajiwa kuhudumia aila za raia wa Sahara ya Magharibi, waliotengwa na jamii zao na ambao sasa huishi katika kambi za wahamiaji ziliopo Tindouf, Algeria.

Mwezi Januari Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) lilipendekeza lipatiwe dola milioni 3.5 kuendelea kuhudumia ziara za familia pamoja na huduma za simu miongoni mwa WaSaharawi 90,000 wanaoishi kwenye kambi za wahamiaji mipakani Algeria. Huduma hizi, zilizoanzishwa 2004, ziliziwezesha aila husika kuzuru jamaa zao waliopo Sahara ya Magharibi, na vile vile kuwapatia fursa ya kuwasiliana na jamii hizo kwa kutumia njia ya simu, kutokana na misaada ya fedha iliosimamiwa na UNHCR.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter