Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Naibu KM wa UM anasailia matatizo ya kimataifa na Redio ya UM

Naibu KM wa UM anasailia matatizo ya kimataifa na Redio ya UM

Wiki hii wasikilizaji Idhaa ya Kiswahili ya Redio ya UM ilibahatika kupata fursa ya kufanya mahojiano maalumu na Naibu KM wa UM, Asha-Rose Migiro kwenye studio zetu. Naibu KM Migiro alisailia mada kadha wa kadha zinazoambatana na shughuli za UM, ikijumuisha utekelezaji wa Malengo ya Milenia ya Maendeleo (MDGs)katika mataifa masikini, suala la Darfur, mageuzi katika UM, udhibiti wa mabadailiko ya hali ya hewa na kadhalika.

Kwa sababu ya wakati mdogo tulionao wa kipindi, wiki hii tumelazimika kukupatieni dokezo tu ya mazungumzo yetu na Naibu KM. Tunatumai wiki zijazo kukupatieni mahojiano kamili. NKM Migiro alianza mahojiano yetu kwa maelezo juu ya mfumo wa Tume ilioundwa karibuni na KM Ban Ki-moon, ya kuongoza utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya MDGs katika mataifa ya Afrika yaliopo kusini ya Sahara, nchi ambazo imeripotiwa bado zinazorota na kupwelewa kwenye juhudi za kupunguza ufukara na hali duni kwenye maeneo yao.

Sikiliza mahojiano kwenye idhaa ya mtandao.