Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zowezi la kuwapokonya silaha wapiganaji katika DRC

Zowezi la kuwapokonya silaha wapiganaji katika DRC

Awamu ya tatu ya kuwapokonya silaha, na kuwarudisha katika maisha ya kiraia au kujiunga na jeshi la taifa, kwa ajili ya makundi matatu ya waasi huko Ituri, ilianza mapema mwezi wa Julai.

Mradi huo unaosimamiwa na shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, unapanga kuwapokonya silaha karibu wapiganaji elfu nne mia tano, na kuwapatia mafunzo ya kazi na kuwarudisha katika maisha ya kiraia kwa wale wanaotaka na wengine wana andikishwa katika jeshi la taifa. Nilizungumza na Bi Providence Mukarukundo, mratibu wa kuwahamasisha raia na wapiganaji katika UNDP na kumuliza kwanza juu ya awamu hiyo ya tatu.