Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jopo juu ya Mashariki ya Kati ya unga mkono mwito wa rais wa Marekani.

Jopo juu ya Mashariki ya Kati ya unga mkono mwito wa rais wa Marekani.

Jopo la kidiplomasia la pande nne juu ya Mashariki ya Kati, limemunga mkono wiki hii, Rais wa Marekani George Bush, kwa kutoa mwito wa kuitishwa mkutano wa Kimataifa baadae mwaka huu.

Jopo hilo la wajumbe kutoka Umoja wa Mataifa, Jumuia ya Ulaya, Rashia na Marekani lilitoa taarifa kunga mkono mwito huo baada ya mkutano wa mawaziri wa mambo ya nchi za njee wa pande zote, pamoja na waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair, mjini Lisbon Ureno. Jopo lilikubaliana kwamba mkutano kama huo utaweza kuzipatia pande zinazohusika msaada wa kidiplomasia katika mazungumzo kati ya Israel na Palestina na majadiliano kuelekea kuundwa kwa taifa la wa-Palestina. Jopo limemkaribisha Bw Blair kua mjumbe maalum wa Jopo na walijadili juu ya kazi zinazomkabili.