Skip to main content

Ban Ki-moon apongeza mazungumzo juu ya Darfur

Ban Ki-moon apongeza mazungumzo juu ya Darfur

Katibu mkuu wa UM amepongeza matokeo ya mkutano wa kimataifa ulohudhuriwa na pande zote juu ya hali huko Darfur wiki hii. Wajumbe maalum walopewa jukumu la kufufua utaratibu wa amani wa Darfur, Dk. Salim Ahmed Salim wa Jumuia ya Afrika, AU na Bw Jan Eliasson wa UM, walitisha mkutano wa siku mbili jinni Tripoli, hapo Julai 15 na 16.

Katibu mkuu anasema, “mkutano umethibitisha tena uungaji mkono mkubwa wa jukumu la uwongozi wa AU na UM katika majadiliano ya kufikia suluhisho la kudumu kwa mzozo wa Darfur. Mataifa 18 na mashirika ya kimataifa yaliyoshiriki, yameahidi ungaji mkono kamili. Wajumbe maalum wataitisha mkutano mwengine mjini Arusha, Tanzania, mwezi ujao ili kuanza majadiliano ya kisiasa na pande zote zinazohusika.