Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jedwali ya kukamilisha kesi kwa wakati imeripotiwa rasmi na ICTR

Jedwali ya kukamilisha kesi kwa wakati imeripotiwa rasmi na ICTR

Erik Mose, Raisi wa Mahakama ya Kimataifa juu ya Rwanda (ICTR), ametuma ripoti kwa Baraza la Usalama inayoelezea mpango wa matarajio ya kukamilisha kesi zake kwa wakati.

Ndani ya ripoti iliashiriwa ya kwamba itakapofika mwisho wa 2008 Mahakama ya ICTR inatarajia kukamilisha hukumu ya kesi za watuhumiwa 65 hadi 70. Hivi sasa Mahakama imeshatoa hukumu ya watu 33, licha ya kuwa vile vile kuna watuhumiwa 18 wengineo ambao bado wapo huru na hawajashikwa na kupelekwa mahakamani kukabili mashtaka.