Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MONUC imechukizwa na mauaji ya mwanahabari wa Redio Okapi

MONUC imechukizwa na mauaji ya mwanahabari wa Redio Okapi

Mwakilishi Maalumu wa KM katika JKK (DRC), William Swing ametoa taarifa yenye kulaani vikali mauaji ya Serge Maheshe mwanahabari wa Redio Okapi, steshini ambayo hudhaminiwa na UM pamoja na Shirika la Kiswiss la Taasisi ya Hirondelle.

Mnamo tarehe 13 Juni marehemu Maheshe alipigwa risasi na watu wawili, katika mji wa Bukavu, mashariki ya JKK wakati alipokuwa anajaribu kuingia kwenye gari lenye alama rasmi ya UM. Kwa mujibu wa taarifa za Shirika la ulinzi wa amani katika JKK (MONUC) polisi wa taifa wamewashika watu 15 waliotuhumiwa kuhusika na mauaji hayo.