Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tume ya Baraza la Usalama imeanza safari rasmi ya kuzuru mataifa matano Afrika

Tume ya Baraza la Usalama imeanza safari rasmi ya kuzuru mataifa matano Afrika

Ujumbe maalumu wa Baraza la Usalama unaoongozwa na Balozi wa Uingereza Emyr Jones-Parry pamoja na Balozi Dumisani Khumalo wa Afrika Kusini uliondoka New York Alkhamisi, tarehe 14 Juni (2007) kuanza ziara ya wiki moja kutembelea mataifa matano katika Afrika, ikiwemo Ethiopia na Sudan.

Watakapokuwapo Addis Ababa, Ethiopia mnamo tarehe 16 Juni watafanya mazungumzo na Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika (AU) pamoja na kukutana kwa mashauriano na maofisa wa Serekali ya Ethiopia, halkadhalika. Ujumbe wa Baraza la Usalama unatazamiwa kuwepo Khartoum tarehe 17 Juni ambapo watakutana kwa mazungumzo na Raisi Omar al-Bashir wa Sudan pamoja na maofisa wa hadhi za juu wa Serekali na vile vile kujumuisha wafanyakazi wa Shirika la Operesheni za Amani za UM Sudan (UNMIS). Baada ya hapo tume ya Barza la Usalama itaelekea Accra, Ghana; Abidjan, Cote d'Ivoire na kumalizia ziara yao ya Afrika mjini Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kabla ya kurejea New York mnamo tarehe 21 Juni.