Skip to main content

Umoja wa Mataifa kumkumbuka KM wa zamani Kurt Weldheim

Umoja wa Mataifa kumkumbuka KM wa zamani Kurt Weldheim

Alkhamisi, tarehe 14 Juni UM ulipokea taarifa ya kuhuzunisha kuhusu kifo cha aliyekuwa KM wa nne wa UM na pia Raisi wa zamani wa Austria, Kurt Waldheim. Risla ya KM wa sasa Ban Ki—moon juu ya msiba huo ilikumbusha ya kwamba Marehemu Waldheim alipata fursa ya kuutumikia UM kuanzia 1972 hadi 1981, katika kipindi ambacho, alitilia mkazo, ni muhimu sana katika historia ya taasisi hii ya kimataifa.

UM ulipandisha bendera ya UM pekee, nusu mlingoti, kwenye Makao Makuu kumkumbuka KM Waldheim wakati bendera nyenginezo za Mataifa Wanachama hazikupeperushwa mwisho wa wiki.