Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KM na wafanyabiashara waahidi mchango wao kukabiliana na UKIMWI

KM na wafanyabiashara waahidi mchango wao kukabiliana na UKIMWI

KM Ban Ki-moon pamoja na wafanyabiasahara wa sekta ya binafsi waliohudhuria kikao maalumu kilichofanyika Makao Makuu kuzingatia juhudi za kupiga vita UKIMWI, kifua kikuu na malaria wamethibitisha kwenye taarifa zao mbalimbali umuhimu na ulazima wa kuimarisha ushirikiano wa pamoja kati ya sekta ya umma na sekta binafsi ili kuweza kudhibiti bora maradhi haya thakili yenye kusumbua umma wa kimataifa.

KM Ban alipongeza kidhati ule mchango wa Jumuiya ya Wafanya Biashara Ulimwenguni au Jumuiya ya GBC, ambayo hujumuisha makampuni 220 ya kimataifa -kwa mchango wao maridhawa uliodhamiriwa kutumiwa kwenye kadhia za kudhibiti na kufyeka UKIMWI duniani.