KM na Baraza la Usalama kuyapongeza maafikiano ya amani Burundi
Raisi wa Baraza la Usalama kwa mwezi Juni, Balozi Johan Verbeke wa Ubelgiji aliwaambia waandishi habari kuwa wawakilishi wa Baraza hilo wanayaunga mkono maafikiano ya mazungumzo ya 17 Juni yaliokubaliwa Dar-es-Salaam, Tanzania baina ya Raisi wa Burundi Pierre Nkurunziza pamoja na kiongozi wa kundi la wanamgambo la Palipehutu-FNL, Agathon Rwasa.
Kadhalika Kamisheni ya Ujenzi wa Amani iliobuniwa na UM kuyasaidia mataifa yanayofufuka kutoka athari za vurugu na mapigano kutoteleza na kurejea kwenye mazingira ya uhasama, imeidhinisha mfumo wa kuihusisha Burundi, UM na wabia wengineo wa kimataifa kwenye juhudi za pamoja za kuimarisha amani kwenye eneo hili la Afrika.