Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mazungumzo ya kuleta amani Sahara Magharibi kurudiwa tena Agosti

Mazungumzo ya kuleta amani Sahara Magharibi kurudiwa tena Agosti

Mazungumzo ya siku mbili yaliodhaminiwa na UM, juu ya Sahara ya Magharibi, yaliofanyika wiki hii katika kitongoji cha Manhasset, New York kati ya Morocco na Chama cha Ukombozi wa Sahara ya Magharibi cha Frente Polisario, na ambayo vile vile yalijumuisha wawakilishi wa mataifa jirani na Sahara Magharibi ya Algeria na Mauritania, yalikamilishwa kwa makubaliano kuwa makundi husika yatarejea tena New York mnamo wiki ya pili ya Agosti kuendelea na majadiliano yao ya kutafuta suluhu ya kudumu na kuriidhisha juu ya mgogoro wa eneo hili la Afrika Kaskazini.

Mazungumzo yaliongozwa na Peter van Walsum, Mjumbe wa KM kwa Sahara ya Magharibi.