Fafanuzi za kikao cha 51 cha Kamisheni ya CSW kuhusu haki za wanawake

5 Aprili 2007

Kamisheni ya Baraza Kuu la UM juu ya Hadhi na Haki za Wanawake, au Kamisheni ya CSW, karibuni ilikutana kwenye Makao Makuu ya UM mjini New York, na kuzingatia utaratibu wa kuchukuliwa na nchi wanachama kuharakisha utekelezaji wa ile mikataba na miradi iliopitishwa na kuidhinishwa kimataifa, inayohusu haki za wanawake, ili kulipatia fungu hili la kijinsia ulinzi halali dhidi ya vitendo vya kibaguzi.~

Rachel B. Dzombo, Katibu wa Kudumu wa Wizara ya Jinsia, Riadha, Utamaduni na Huduma za Jamii katika Kenya alikuwa miongoni mwa wajumbe kutoka Afrika Mashariki waliohudhuria kikao cha 51 cha Kamisheni ya CSW, na alikubaliana na uchambuzi wa Naibu KM juu ya hadhi ya wanawake ulimwenguni na mzoroto uliopo ulimwenguni katika kuwatekelezea haki zao kama inavyostahiki. Kwenye mazungumzo niliyoyafanya kwenye studio zetu Bi Dzombo, anatufafanulia zaidi maoni yake kuhusu namna mijadala ya Kamisheni ya CSW ilivyoendeshwa, na pia kusailia harakati za kimataifa zinazohitajika kuwatekelezea wanawake na watoto wa kike haki halali za kimsingi.

Sikiliza idhaa ya mtandao kwa mahojiano kamili.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter