Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjumbe wa Kenya achambua kikao cha mwaka cha Kamisheni ya CSW

Mjumbe wa Kenya achambua kikao cha mwaka cha Kamisheni ya CSW

Kamisheni ya Haki za Wanawake, au Kamisheni ya CSW, ilikutana kwa muda wa wiki mbili kwenye Makao Makuu, mjini New York, katika kikao cha mwaka kuanzia tarehe 26 Februari hadi tarehe 09 Machi (2007). Kikao cha 2007 ni cha 51.

Bibi Rachel Dzombo, Katibu wa Kudumu wa Wizara ya Jinsiya, Riadha, Utamaduni na Huduma za Jamii kutoka Kenya alikuwa miongoni mwa maelfu ya wale wajumbe wa kimataifa waliohudhuria kikao cha Kamisheni ya Haki za Wanawake, au Kamisheni ya CSW. Kwenye mahojiano aliyokuwa nayo na Idhaa ya Redio ya UM alitufafanulia mawazo yake kuhusu shughuli za mkutano na matarajio yake kwa siku za usoni.

Kwa ripoti kamili sikiliza idhaa ya mtandao.