Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO yatahadharisha hatari ya nzige kwenye eneo la kaskazini-mashariki ya Afrika

FAO yatahadharisha hatari ya nzige kwenye eneo la kaskazini-mashariki ya Afrika

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) limetoa mwito maalumu kwa nchi za kaskazini-mashariki ya Afrika kuongeza uchunguzi wao na operesheni za kudhibiti hatari ya nzige, hususan kwenye maeneo ya mwambao wa Bahari Nyekundu katika Eritrea na Sudan na katika kaskazini-magharibi ya Usomali.

FAO pamoja na Shirika la Udhibiti wa Nzige wa Jangwani kwa Afrika Mashariki (DLCO-EA) yameanzisha operesheni za pamoja za anga, wiki hii, kwenye mwambao wa Bahari Nyekundu, mipakani kati ya Sudan na Eritrea, zilizokusudiwa kuyakinga maeneo ya kaskazini-mashariki ya Afrika dhidi ya makundi ya nzige haribifu yasije yakafumka na kuanza kuangamiza mazao na malisho katika eneo hilo la Pembe ya Afrika.