Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM imeanzisha tena huduma za kihali baada ya fujo kufifia DRC

UM imeanzisha tena huduma za kihali baada ya fujo kufifia DRC

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti ya kuwa hali ya vurugu na mapigano yaliofumka karibuni mjini Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), baina ya vikosi vya Serekali na wafuasi wenye silaha wa aliyekuwa Naibu-Raisi Jean-Pierre Bemba, imeanza kufifia wiki hii na kuyawezesha mashirika yanayohudumia misaada ya kiutu fursa ya kuendeleza shughuli za kutathminia hali, kwa ujumla, na vile vile kukidhia mahitaji ya umma ulioathirika na mapigano.

Shirika la Afya Duniani (WHO)limeshagawa tani tatu za metriki za dawa muhimu za matibabu, pamoja na zana za tiba ya upasuaji, na vile vile plasta na shuka safi za kutumiwa katika mahospitali.

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dahrura (OCHA)ilihimiza jumuia ya kimataifa kuyapatia ulnzi kinga na hifadhi bora wale raia dhaifu, wakijumuisha familia na wale watu wanaotegemea wafuasi wa Bemba pamoja na watoto wa mitaani waliowekwa vizuizini, na kuhakikisha kuna ulinzi dhidi ya udhalilishaji wa kijinsia na ukiukaji wa jumla wa haki za kibinadamu.