Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapigano mapya yahatarisha mfumo wa amani Usomali, aonya Ban Ki-moon

Mapigano mapya yahatarisha mfumo wa amani Usomali, aonya Ban Ki-moon

KM Ban Ki-moon ameripoti, kwa kupitia msemaji wake, ya kwamba ana wasiwasi juu ya kukithiri karibuni kwa hali ya mapigano katika mji wa Mogadishu, mgogoro ambao ulisababisha msiba wa vifo kadha wa kadha vya raia.

KM alishtumu kwenye risala yake, hususan yale matumizi ya vifaru, mizinga mikubwa na ndege dhidi ya yale maeneo wanamoishi raia, hali ambayo alionya kama haijadhibitiwa haraka huenda ikafumua tena utaratibu wa amani na utulivu nchini Usomali.