Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti ya UNICEF yalaani 'utalii wa hasharati' katika mwambao wa Kenya

Ripoti ya UNICEF yalaani 'utalii wa hasharati' katika mwambao wa Kenya

Ripoti ya UNICEF iliyozingatia masuala yanayoambatana na kile kinachotambuliwa kama \'utalii wa uasherati\' katika Kenya imefichua ya kwamba karibu asilimia 30 ya vijana wa kike, ikijumuisha vijana 10,000 hadi 15,000 katika maeneo ya mwambao ya Malindi, Mombasa, Kilifi na Diani hushiriki kwenye vitendo karaha vya ukahaba na umalaya.

Agnetta Merikao wa Ofisi ya UNICEF-Nairobi alitupatia dokezo ya ripoti hiyo katika mahojiano ya redio na Ofisi ya Habari ya UM ya Nairobi.

Sikiliza ripoti kamili kwenye idhaa ya mtandao.