Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Iraq iendelee kufanyia marekebisho makampuni ya ulinzi:UM

Iraq iendelee kufanyia marekebisho makampuni ya ulinzi:UM

Kundi moja la wataalamu wa haki za binadamu kutoka Umoja wa Mataifa linasema kuwa huku visa vinavyohusiana na walinzi wa kibinafasi na makampuni ya ulinzi vikiendelea kupungua nchini Iraq katika miaka ya hivi majuzi, serikali inastahili kufanyia makadiliko na kuchunguza shughuli zao.

Kupungua kwa idadi ya visa kumetokana na kupungua kwa shughuli zinazohusiana na jeshi za kampuni hizo nchini Iraq , usimamizi mkali wa utawala nchini Iraq na jitihada za Marekani za kusimamia shughuli za makampuni yake ya kutoa ulinzi ya kibinafsi yaliyo nchini Iraq.

Kati ya mapendekezo ya kundi hilo ni kuwa wataalamu hao wameitaka serikali ya Iraq kuanza kutekeleza sheria za kusimiamia makampuni ya ulinzi ambazo zimekuwa tangu mwaka 2008.