Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mazungumzo ya upatanishi juu ya Sahara ya Magharibi yamemalizika, yatarudiwa tena Machi

Mazungumzo ya upatanishi juu ya Sahara ya Magharibi yamemalizika, yatarudiwa tena Machi

Duru ya tatu ya mazungumzo ya siku mbili yalioandaliwa na UM kutafuta suluhu ya kuridhisha juu ya tatizo la Sahara ya Magharibi, yaliofanyika kwenye mji wa Manhasset, katika Jimbo la New York yamemalizika kati ya wiki. Makundi yote husika na mzozo huu yalitoa taarifa ya pamoja baada ya mkutano kukamilishwa iliosema makundi husika yamekubaliana kukusanyika tena mwezi Machi mahali hapo hapo pa Manhasset na yameahidi kuwa yazingatia kwa hamasa zaidi na kiwango kikubwa yale masuala yaliotatanisha upatanishi wao.

Mkutano ulihudhuriwa na wajumbe wa Chama cha Ukombozi cha Frente Polisario, Morocco pamoja na wawakilishi wa mataifa jirani ya Algeria na Mauritania na majadiliano yaliongozwa na Mwakilishi Maalumu wa KM kwa Sahara ya Magharibi, Peter van Walsum.