Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa za hapa na pale

Taarifa za hapa na pale

Inga-Britt Ahlenius, Mkuu wa Idara ya UM ya Uchunguzi wa Makosa ya Udanganyifu na Ulaji Rushwa (OIOS) alikutana na waandishi habari wa kimataifa waliopo Makao Makuu na kuwazindua ya kwamba moja ya shuruti muhimu zilizowekwa kudhibiti bora utekelezaji wa shughuli za UM, miongoni mwa watumishi wa taasisi hii ya kimataifa ni kuhakikisha kunakuwepo uwazi kwenye utekelezaji wa majukumu yao ya kazi, na pia uwajibikaji unaoridhisha, hususan ilivyokuwa wafanyakazi hawa wanaitumikia taasisi maalumu ya kimataifa yenye mazingira yasio ya kikawaida na ya aina pekee.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limedhaminia shirika mkutano maalumu unaofanyika Addis Ababa, Ethiopia kuzingatia taratibu za kurekibisha tiba ya UKIMWI, na kuyasaidia zaidi kihali yale mataifa yenye upungufu wa wahudumia afya, hasa katika Afrika, kikao ambacho kinahudhuriwa na wajumbe 350 wanaowakilisha wizara za afya, viongozi wa afya ya jamii na wataalamu magwiji wanaohusika na UKIMWI.

[na hatimaye] KM Ban Ki-moon amearipoti kwamba atahudhuria ule mkutano wa siku mbili ulioandaliwa na Taasisi ya Ushirikiano wa Tamaduni na Mila Zinazokhitalifiana, utakaofanyika kwenye mji wa Madrid, Uspeni kuzingatia nidhamu za kuziba pengo liliojiri kimataifa kati ya Ustaarabu wa KiIslam na Utamaduni wa Mataifa ya Magharibi.