Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahitaji ya chakula kuongezeka katika JKK Mashariki

Mahitaji ya chakula kuongezeka katika JKK Mashariki

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) leo limetoa onyo maalumu lenye kutahadharisha kwamba limekabiliwa na tatizo la upungufu mkubwa wa akiba ya chakula inayotakiwa kuhudumia makumi elfu ya raia wanaokimbia mapigano yaliofumka mashariki, katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK).