Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waeleza wasiwasi kuhusu mapigano Libya

UM waeleza wasiwasi kuhusu mapigano Libya

Pakua

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya (UNSMIL), umesema unafuatilia kwa masikitiko makubwa hali tete ndani na karibu na mji wa Tamanhint, ambako mapigano bado yanaendelea kuripotiwa.

Aidha, Umoja wa Mataifa umeeleza kutikwa wasiwasi na athari za machafuko hayo kwa maisha ya raia wa kusini mwa Libya.

UNSMIL imesema kuwa imepokea ripoti za uhaba wa chakula, maji, dawa, pamoja na kutitizwa kwa huduma za nguvu za umeme, na pia kwamba familia zinakimbia makwao huko Tamahnint na kwenda Sabha na Ubari.

Photo Credit
Msichana huyu akichunugia dirishani akiwa Benghazi Libya ambako machafuko yamekumba sehemu mbali mbali.(Picha:UNSMIL/Maktaba)