Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

03 JULAI 2024

03 JULAI 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia tunaangazia maadhimisho ya tatu ya siku ya lugha ya Kiswahili duniani maudhui yakiwa nafasi ya elimu ya sanaa. Makala tunatupeleka nchini Ghana kumulika umahiri wa wanafunzi wa Kiswahili, na mashinani tunakupeleka nchini China kusikia ujumbe wa mdau kuhusu lugha y aKiswahili.

  1. Hii leo hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa kunafanyika maadhimisho ya tatu ya siku ya lugha ya Kiswahili duniani maudhui yakiwa nafasi ya elimu ya sanaa katika kukuza na kuendeleza lugha ya Kiswahili. Maadhimisho haya yanafanyika tarehe 3 kwa kuwa siku yenyewe ya Kiswahili duniani yaani tarehe 7 Julai itaangukia siku ya Jumapili na Anold Kayanda anafuatilia kwenye maadhimisho hayo.
  2. Tukiendlea na maadhimisho ya Siku ya Kiswahili duniani mwenzetu Assumpta Massoi naye anafuatilia maadhimisho hayo na ametuandalia taarifa pamoja na mazungumzo yake na aliyehudhuria maadhimisho hayo.
  3. Katika makala Bosco Cosmas anatupeleka nchini Ghana kumulika umahiri wa wanafunzi wa Kiswahili.
  4. Na katika mashinani Siku ya Kimataifa ya Lugha ya Kiswahili inaadhimishwa Jumapili Julai 7, Masika Yang, Mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) anatoa ujumbe kuhusu lugha ya Kiswahili.

Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu! 

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
9'58"