Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwaka 2020 UN imeteua wanawake viongozi 20 na 2021 utafuata nyayo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amewateua wanawake 20 katika nyadhifa za juu katika mwaka 2020
UN
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amewateua wanawake 20 katika nyadhifa za juu katika mwaka 2020

Mwaka 2020 UN imeteua wanawake viongozi 20 na 2021 utafuata nyayo

Wanawake

Mwaka 2020 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameteua wanawake 20 kushikilia nyadhifa za juu za uongozi.

Wanawake tisa kati ya hao waliteuliwa katika nafasi za kisiasa au mipango ya amani mashinani. Na kati ya wanawake hao 9 wanatoka Afrika, 7 bara amerika na visiwa vya Caribbea, 3 bara Ulaya na 1 kutoka Asia. Basi leo tunawamulika wanawake hao 9 kutoka bara la Afrika ambao usikose kuwafuatilia mwaka 2021.

 

Naibu mwakilishi maalum kwa ajili ya ukanda wa Afrika Magharibi na Sahel (UNOWAS)
UNODC
Naibu mwakilishi maalum kwa ajili ya ukanda wa Afrika Magharibi na Sahel (UNOWAS)

 

Giovanie BIHA
Nchi: Burundi
Wadhifa: Naibu mwakilishi maalum kwa ajili ya ukanda wa Afrika Magharibi na Sahel (UNOWAS)
Ngazi: Msaidizi wa Katibu Mkuu


Bi. Biha ana uzoefu wa kina kwenye Umoja wa Mataifa kwani ameshawahi kushikilia nyadhifa mbalimbali kwenye shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP, kwenye kamisheni ya masuala ya kiuchumi kwa ajili ya Afrika ECA, kama naibu katibu mkuu mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake UN Women, kama mkurugenzi msimamizi, na pia amefanya kazi kwenye secretariat ya Umoja wa Mataifa.
Hivi karibuni kabisa Bi. Biha alikuwa naibu mkurugenzi wa ofisi ya kuratibu shughuli za maendeleo (BCAD).
Kabla ya kujiunga na Umoja wa Mataifa alishjikilia nafasi ya juu kwenye Benki kuu ya Burundi na Benki ya biashara na uwekezaji.

Mkurugenzi wa ofisi ya UNDP kanda ya nchi za Kiarabu
Screen capture
Mkurugenzi wa ofisi ya UNDP kanda ya nchi za Kiarabu

 

Khalida BOUZAR
Nchi: Algeria
Wadhifa: Mkurugenzi wa ofisi ya UNDP kanda ya nchi za Kiarabu 
Ngazi: Msaidizi wa Katibu Mkuu


Kabla ya kuteuliwa Khalida Bouzar alikuwa mkurugenzi wa kanda ya Mashariki ya karibu, Afroika Kaskazini na Ulaya wa mfuko wa kimataifa kwa ajili ya maendeleo ya kilimo IFAD tangu mwaka 2012 ambako alianzisha na kusimamia mipango na operesheni kwa kiwango kikubwa.
Ana uzoefu wa Zaidi ya miaka 35 ya uongozi katika kiwango cha kimataifa na kitaifa, ikiwemo miaka 25 ndani ya mfumo wa Umoja wa Mataifa.
Elimu yake, utalaam wake, uzoefu wake, ujuzi wake na masuala anayopendelea yanajumuisha masuala mbalimbali ya maendeleo, ikiwemo maendeleo endelevu, maendeleo vijijini, mazingira, mabadiliko ya tabianchi, uhamiaji, uchumi na viwanda, na kwa kiasi kikubwa katika mazingira magumu na migogoro.
Bi. Bouzar ana ueleewa wa kina wa ukanda wa mataifa ya Kiarabu pamoja na shughuli za Umoja wa Mataifa na mashirika yake katika ngazi ya kimataifa, kikanda na kitaifa, iwe ni sera, proframu na usimamizi na operesheni.
Ana shahada ya udaktari au uzamivu katika masuala ya sayansi kutoka chou kikuu cha masuala ya sayansi cha Pierre et Marie Curie mjini Paris Ufaransa. 
Na anazungumza kwa ufasaha lugha za Kiingereza, Kiarabu na Kifaransa.

Naibu mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu (UNFPA)
UNFPA
Naibu mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu (UNFPA)

 

Diene KEITA 
Nchi: Guinea
Wadhifa: Naibu mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu (UNFPA)
Ngazi: Msaidizi wa Katibu Mkuu 


Mpaka wakati anateuliwa Dienne Keita alikuwa waziri wa Guinea wa mahusiano na ushirikiano wa Afrika.
Bi.Keita anakuja katika wadhifa huu mpya na uzoefu wa karibu miaka 30 katika mfumo wa Umoja wa Mataifa.
Mwaka 1990 alikuwa afisa wa program kwenye shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP mjini New York, kabla ya kushika nyadhifa nyingine mbalimbali za ngazi ya juu ya kitaifa ikiwemo kuwa naibu mwakilishi wa UNDP na kaimu mwakilishi.
Bi. Keita alijiunga na UNFPA mwaka 2006 kama mwakilishi nchini Mauritania. Na kisha akahudumu kama mwakilishi wa shirika hilo Benin, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC na Nigeria, na baadaye programbu mbili kubwa Zaidi za UNFPA duniani.
Wakati akiwa bado na UNFPA Bi. Keita alifanyakazi kama mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Mauritania, Benin na DRC ambako alisimamia mfumo wa Umoja wa Mataifa.
Katika miaka yote ya uchapaji kazi wake Bi. Keita amefanyakazi na kujikita kwa kina katika masuala ya uwezeshaji wa wanawake na vijana, ukuaji jumuishi, masuala ya idadi ya watu, maendeleo endelevu ya binadamu, afya ya uzazi, unyanyasaji wa kijinsia na masuala ya kibinadamu.
Bi. Keita anazungumza kwa ufasaha Kifaransa na Kiitaliano. Pia ana shahada ya udaktari au ya uzamivu katika masuala ya sheria , ana stashahada ya masomo ya sheria za uchumi wa kimataifa na maendeleo na ana shahada ya pili ya masuala ya ushusiano wa kimataifa kutoka kwenye chou kikuu cha 1 Pantheon Sorbonne mjini Paris Ufaransa.

Elizabeth Maruma Mrema kutoka Tanzania ameteuliwa na Katibu Mkuu wa UN kuwa Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya Mkataba wa Kimatafa wa Bayonuai ya kibaiolojia, CBD.
UNEP
Elizabeth Maruma Mrema kutoka Tanzania ameteuliwa na Katibu Mkuu wa UN kuwa Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya Mkataba wa Kimatafa wa Bayonuai ya kibaiolojia, CBD.

 

Elizabeth Marum MREMA
Nchi: Tanzania
Wadhifa: Katibu Mtendaji wa secretariat ya Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya bayoanui (CBD) 
Ngazi: Msaidizi wa Katibu Mkuu


Mpaka uteuzi wake ulipothibitishwa Bi. Mrema alikuwa akifanyakazi kama kaimu Katibu Mkuu wa sekretariati ya ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya bayoanuai (CBD) tangu Desemba 2019. 
Kabla ya hapo alikuwa mkurugenzi wa idara ya sheria ya shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira UNEP jijini Nairobi Kenya.
Akiwa na Zaidi ya miongo miwili ya uzoefu kwenye Umoja wa Mataifa , Bi. Mrema ana uzoefu wa kina wa sheria  na sera za kimataifa za masuala ya mazingira na utekelezaji wa program za mazingira na maendeleo endelevu pamoja na ufahamu mkubwa wa michakato ya ushirikiano wa kimataifa.
Kuanzia mwaka 2009-2012 alikuwa katibu mtendaji wa UNEP kwenye sekretarieti ya mkataba kuhusu uhifadhi wa aina ya viumbe vya wanyamapori vinavyohama, na pia alishika cheo cha kaimu katibu mtendaji wa UNEP/ASCOBANS ambayo ni makubaliano ya mkataba wa viumbe vidogo kwenye bahari za Baltic, Kaskazini Mashariki mwa Atlantic na bahari ya Kaskazini mwa Ireland.
Na pia aliwahi kuwa kaimu katibu mkuu wa UNEP kuhusu makubaliano ya nyani , zote hizo zikiwa na makao yake mjini Bonn Ujerumani.
Nas kabla ya kujiunga na UNEP, Bi. Mrema alifanyakazi katika wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa nchini Tanzania.
Katika muda aliofanyakazi wizara ya mambo ya nje Bi. Mrema pia alifundisha masomo ya sheria za kimataifa za umma na diplomasia ya mikutano katika kitruo cha uhusiano wa kimataifa na diplomasia cha Tanzania.
Bi. Mrema ana shahada ya uzamili ya masuala ya sheria kutoka chou kikuu cha Dalhousie Halifax Canada, ana shahada ya pili ya uhusiano wa kimataifa na diplomasia kutoka kwenye chou cha uhusiano wa kigeni na diplomasia Dar es Salaam Tanzania, na ana shahada ya masuala ya sheria kutoka chou kikuu cha dar es salaam Tanzania.

Mshauri maalum kuhusu kuzuia mauaji ya kimbari Ngazi: Naibu Katibu Mkuu
Screen capture
Mshauri maalum kuhusu kuzuia mauaji ya kimbari Ngazi: Naibu Katibu Mkuu

 

Alice Wairimu NDERITU
Nchi: Kenya
Wadhifa: Mshauri maalum kuhusu kuzuia mauaji ya kimbari
Ngazi: Naibu Katibu Mkuu


Bi. Nderitu ni sauti inayotambulika katika nyanja yaulinzi wa amani na kuzuia machafuko.
Amekuwa mpatanishi na mshauri wa ngazi ya juu katika michakato kwenye jamii nchini mwake lakini pia katika sehemu mbalimbali Afrika. 
Aliwahi kuhudumu kama kamishina wa tume ya kitaifa ya ushirikiano na utangamano nchini Kenya mwaka 2009-2013 na pia alikuwa mwanachama mwanzilishi na mwenyekiti mwenza wa jukwaa la Uwiano la amani, shirika la kuzuia lakini pia linalounganisha utoaji wa tahadhari ya mapema na hatua za mapema nchini Kenya. 
Bi. Nderitu pia ni mwanzilishi wa ‘Community Voices for Peace and Pluralism” mtandao wa wanawake wenye taaluma barani afrika wa kuzuia, kubadili na kutatua machafuko ya kikabila, rangi na kidini kote duniani. 
Bi. Nderitu uzowefu wake kitaifa ni pamoja na kuhudumu kama mkurugenzi wa Elimu kwa ajili ya Haki Fahamu mwaka 2007-2009, mkuu wa mpango wa elimu ya haki za binadamu na kujenga uwezo  kwa ajili ya tume ya kitaifa ya haki za binadamu nchini Kenya na kamati ya haki za binadamu kati yam waka 1999-2007. 
Pia amewahi kuwa mtafiti na msimamizi wa huduma za magereza Kenya , kwenye wizara ya mambo ya ndani mwaka 1992-1999. 
Anahudumu kama mjumbe wa kamati ya kityaifa ya kuzuia na kuadhibu uhalifu wa mauaji ya kimbari, uhalifu wa vita, uhalifu dhidi ya binadamu na aina zote za ubaguzi, kwenye mtandao wa Muungano wa Afrika wa Wanawake wa Afrika