Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pande kinzani nchini Libya zakutana kujadili hatua za usitishaji uhasama:UNSMIL 

Stephanie Williams, kaimu mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya katika kamati ya (5+5) Ghadames nchini Libya.
UNSMIL
Stephanie Williams, kaimu mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya katika kamati ya (5+5) Ghadames nchini Libya.

Pande kinzani nchini Libya zakutana kujadili hatua za usitishaji uhasama:UNSMIL 

Amani na Usalama

Nchini Libya pande mbili kinzani katika mzozo unaoendelea zimekutana kwa mara ya kwanza kujadili jinsi ya utekelezaji wa usitishaji uhasama nchi nzima.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNSMIL Jumanne jioni , mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo, wawakilishi wa jeshi kutoka serikali ya mkataba wa kitaifa (GNA) na jeshi la kitaifa la Libya (LNA) wamekutana mjini Ghadames Kusini mwa nchi hiyo. 

UNSMIL imesema “Washiriki wataanzisha majadiliano kuhusu utekelezaji wa makubaliano ya usitishaji uhasama kwa kuanzisha kamati za pamoja na mkakati wa ufuatiliaji na uhakiki wa mchakato huo.” 

Libya imekuwa katika mgogoro tangu mwaka 2011 ilipoangushwa serikali ya aliyekuwa kiongozi wa taifa hilo Muammar Gaddafi na kuzusha pande mbili kinzani za utawala huku GNA ilidhibiti mji mkuu Tripoli na LNA ikidhibiti eneo kubwa Mashariki mwa nchi hiyo. 

Mazungumzo hayo yanayofanyika sanjari na majadiliano mengine yenye lengo la kuileta pamoja nchi hiyo katika uchaguzi wa kitaifa na kufufua uchumi ulioporomoka katika nchi hiyo Tajiri wa mafuta, yamekuja kufutia wajumbe wa pande zote kutia saini kwa makubaliano ya kudumu ya usitishaji uhasama mwezi uliopita mjini Geneva Uswisi.