Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utangamano ni utajiri na si chachu ya mgawanyiko:UNESCO

Watoto nchini Ukaraine wakicheza na bango la SDGs likionyesha watoto kutoka nchi na rangi tofauto kote duniani
UNDP Ukraine/Oleksandr Ratushnyak
Watoto nchini Ukaraine wakicheza na bango la SDGs likionyesha watoto kutoka nchi na rangi tofauto kote duniani

Utangamano ni utajiri na si chachu ya mgawanyiko:UNESCO

Haki za binadamu

Utangamano au mchanganyiko wa watu kutoka maeneo tofauti ni aina ya mfumo wa utajiri na si sababu ya kuleta mgawanyiko amesema mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO katika ujumbe wake maalum wa siku ya kimataifa kwa ajili ya kuvumiliana.

Audrey Azoulay amesema Katika wakati ambao kuna ongezeko la hamasa na itikadi Kali, wakati ambapo jinamizi la chuki linaendelea kutia sumu sehemu ya utu wa binadamu. Ameongeza kuwa “kuvumiliana hakujawahi kuwa na umuhiumu mkubwa kama sasa . kuvumiliana ni zaidi ya kutojali au kutotilia maanani tofauti baina ya wanawake na wanaume , utamaduni na imani, badala yake ni fikra , kutoelewa na kuhitajika kubadili matazamo.”

Mwaka 1996 Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa liliwaalika nchi wanachama katika kusherehekea siku ya kimataifa kila tarehe 16 Novemba ya kila mwaka ambayo pamoja na mambo mengine inachagiza maelewano miongoni mwa tamaduni na watu.Na kwa mwaka huu 2019 siku hiyo itaadhimishwa kesho Jumamosi.

 “utamaduni tofauti ni mfumo wa utajiri na sio sababu ya mgawanyiko”-Audrey Azoulay mkuu wa UNESCO

Amesisitiza kwamba kvumiliana ni kuelewa kwamba kila utamaduni , Zaidi ya tofauti za sasa aua zinazotarajiwa ni sehemu ya ubinadamu wetu na ni lugha ya pamoja ya ubinadamu. Akimnukuu Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan Azouley amesema kwamba “kuvumiliana ni jukwaa linalofanya amani kuwezekana”

Kukabiliana na kutovumiliana

Tangu kuanzishwa kwake shirika la UNESCO limekuwa na lengo la kujenga amani kwa kukabiliana na hali ya kutovumiliana aambayo mara nyingi inasambaratisha jamii zetu, na kupambana na mifumo yote ya ubaguzi wa rangi na ubaguzo mwingine. Akikamilisha ujumbe wake Bi. Azoulay amemtaka kila mtu kusambaza ujumbe wa UNESCO wa kuvumiliana na amani . Amesema kupambana na kutovumiliana

-Kunahitaji sheria: serikali zinawajibika kuhakikisha sheria za haki za binadamu zinatekjelezwa kwa kupiga marufuku uhalifu wa chuki na ubaguzi dhidi ya walio wachache.

-Elimu itolewe na juhudi ziongezwe katika kuelimisha watoto kuhusu kuvumiliana, haki za binadamu na njia zingine za maisha nyumbani na shuleni.

-Lazima kuwe na fursa za kupata tarifa. kuanzishwe sera ambazo zitaweka na kuchagiza uhuru wa vyombo vya Habari na kuruhusu umma kutofautisha baina ya ukweli na maoni.

-Watu binafsi wanapaswa kuelewa uhusiano uliopo baina ya tabia zao, mzunguko wa kutoaminiana na machafuko katika jamiihasa kwa kujiuliza endapo unawasonta vidole watu, unawakataa ambao wako tofauti na wewe au unawalaumu kutokana na matatizo yako.

-Suluhu za kijamii , kuwe na nyenzo zinazohusisha hatua ikiwemo kutokubaliana na propaganda za chuki, kuwekwa makundi ya kukabiliana na matatizo na kuanzisha mtandao mashinani kuonyesha mshikamano na waathirika wa kutovumiliana.