Uhuru wa vyombo vya  habari na kutoa maoni ni mwamba wa kuimarisha serikali

2 Mei 2019

Kuelekea siku ya  uhuru wa vyombo vya habari kesho Mei 3, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema vyombo huru vya habari ni muhimu kwa amani, haki, maendeleo endelevu na haki za binadamu.

Maudhui  ya mwaka huu ni “Vyombo vya Habari kwa Demokrasia: Tasnia ya Habari na Uchaguzi katika Nyakati za Upotoshwaji wa Taarifa.”

Katika ujumbe wake, Bwana Guterres amesema, “hakuna demokrasia iliyo kamilifu bila kupata taarifa kwa uwazi na za kuaminika. Ni msingi wa kujenga taasisi za haki za zisizo na upendeleo, na kuwawajibisha viongozi na kila wakati kueleza mamlaka ukweli.”

Ameongeza kuwa taarifa za uwazi na za kuaminika ni ni muhimu zaidi wakati wa msimu wa uchaguzi, ambayo ndio maudhui ya sik uya Uhuru wa Vyombo vya Habari duniani mwaka hu una kwamba , “taarifa sahihi na si za uongo zinapaswa kuongoza watu wakati wanachagua wawakilishi wao.”

Hata hivyo amesema wakati teknolojia imebadili jinsi tunapokea na kubadilishana taarifa, wakati mwingine inatumika kudanganya maoni ya umma au hata kuchochea ghasia na chuki.

Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2019
UNESCO
Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2019

“Nafasi ya ushiriki wa raia imeendelea kubinywa kote duniani katika kiwango cha kutisha,” amesema Guterres akiongeza kuwa “kadri chuki dhidi vya vyombo vya habari inaongezeka, vivyo hivyo ghasia na manyanyaso dhidi ya wanahabari wakiwemo wanawake.”

Ameesema “nachukizwa sana na ongezeko la matukio ya mashambulizi na utamaduni wa ukwepaji sheria”

Kwa mujibu wa UNESCO, takribani wanahabari 100 waliuawa mwaka 2018 mamia wamefungwa ambapo Katibu Mkuu amesema, “waandishi wa habari wanapolengwa, wanajamii ndio wanaogharimika.”

Kwa mantiki hiyo Bwana Guterres ametoa wito kuwa katika siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari duniani,kila mtu atetee haki za wanahabari ambao juhudi zao zinasaidia kila mtu kujenga dunia bora kwa ajili ya kila mtu.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO Audrey Azoulay amesema uhuru wa vyombo vya habari ni mwamba wa jamii za kidemokrasia.

Kwa mantiki hiyo amesema, “serikali na mataifa zinaimarishika kwa taarifa, mijadala na ubadilishanaji wa maoni. Katika zama za sasa za mwelekeo wa kutoaminiana na kuondoa uhalali wa vyombo vya habari an uandishi wa habari, ni muhimu kuhakikisha kuna uhuru wa kutoa maoni kwa njia ya kubadilishana mawazo na taarifa kupitia taarifa za ukweli.”

 

 

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter