Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Stahamala ni zaidi ya kuvumiliana kwa kutofautiana- UNESCO

Audrey Azoulay Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni,  UNESCO.
UN Photo/Manuel Elías
Audrey Azoulay Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO.

Stahamala ni zaidi ya kuvumiliana kwa kutofautiana- UNESCO

Masuala ya UM

Leo ni siku ya kimataifa ya stahamala ambapo Umoja wa  Mataifa umetumia fursa ya leo kueleza kuwa stahamala si suala la kuvumiliana kwa sababu ya kutofautiana bali ni utayari wa kuheshimu na kukubali watu wengine kwa kuzingatia haki sawa za kibinadamu.

Audrey Azoulay ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni,  UNESCO, shirika ambalo linaratibu siku hii, amesema stahamala ni msingi thabiti wa maadili na siasa ambao unasaidia kuzuia aina mbalimbali za ubaguzi ikiwemo ubaguzi wa rangi.

Nchini Tanzania mbako wananchi wake wana imani tofauti za dini sambamba na makabila, stahamala kwa kiasi kikubwa imekuwa sehemu ya maisha. Sheikh Alhad Musa Salum, Mwenyekiti wa Kamati ya amani inayoundwa na viongozi wa dini mbalimbali nchini humo amesema, "

“Sisi watanzania tuna misingi iliyowekwa na waasisi wa nchi yetu. Leo imefikia wakati viongozi wa kiislam wanacheza mechi ya mpira na viongozi wa kikiristo, tunalikana katika shughuli zetu, sisi tunaenda kwao na wao wanakuja kwetu. Tunasitahimiliana. Viongozi wa dini kote duniani wanaweza kujifunza kwa linaloendelea Tanzania”

Soundcloud

Katika kuadhimisha siku hii, UNESCO inatoa tuzo kwa washindi wa tuzo ya Madanjeet Singh kuhusu uendelezaji wa stahamala na uzuiaji wa ghasia.

Washindi wa mwaka huu ni Manou Barbeu, muandaaji wa filamu kutoka Canada ambaye alianzisha studio ya video na muziki inayotoka eneo moja hadi lingine kwa lengo la kuhamasisha watu kuelewa tamaduni na lugha mbalimbali za jamii ya watu wa asili.

Wengine ni shirika la Coexist Initiative kutoka Kenya ambalo kilichowapatia tuzo hiyo ni kazi yao ya kutetea haki za wanawake na kukabiliana na fikra potofu za kijinsia.