Masuala ya siasa, uchumi , na usalama kutamalaki juwaa la ubia na Somalia
Jukwaa la ushirika na Somalia limeanza leo mjini Brussels Ubelgiji kujadili mambo matatu muhimu ambayo ni siasa, uchumi na usalama.
Katika jukwaa hilo la, siku tatu, serikali ya Somalia pamoja na washirika wake wanaangazia njia zitakazosaidia kudumisha amani na maendeleo katika taifa hilo la pembe ya Afrika. Lisa Filipetto ni mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayosaidia Somalia, UNSOS, ambae anahudhuria mkutano huo. kabla ya kuelekea Ubelgiji kwenye jukwaa hilo ameiambia UN News kuhusu madhumumi kuwepo kwa Umoja wa Mataifa nchini Somalia.
(SAUTI YA LISA FILIPETTO)
“ Kuwepo kwa Umoja wa Mataifa nchini Somalia kuna nia ya kuisadia taifa hilo katika juhudi zake za kuleta amani na utulivu nchini humo ambazo zimegawanyika katika mafungu matatu: siasa, maendeleo ya kiuchumi suala la usalama.”
Ofisi ya UNSOS inasaidia askari 21,000 wa Muungano wa Afrika wa kulinda amani nchini Somalia-AMISOM, wakishirikiana na wanajeshi na polisi wa taifa hilo. Bi Filipetto amesema serikali ya Somalia inajitahidi.
(SAUTI YA LISA FILIPETTO)
“ Lazima tukubali juhudi za serikali ya shirikisho la Somalia kwa kupambana uso kwa uso na changamoto wanazokabiliana nazo katika sekta mbalimbali kwani kisiasia wamepiga hatua kuhusu mfumo wa shirikisho wakilenga uchaguzi mkuu wa 2020, na wanaifufua katiba yao nadhani hilo ni suala muhimu.”
Baadhi ya washirika katika jukwaa hilo la ubia na Somalia ni Umoja wa Mataifa, Muungano wa Ulaya, na Muungano wa Afrika.