Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi wazinduliwa kukabili itikadi kali na zenye ghasia

UNESCO na shirika la kukailiana na ugaidi la Umoja wa Mataifa UNCCT vyazindua mradi wa ubia dhidi ya ugaidi na imani kali kwa vijana
UNESCO
UNESCO na shirika la kukailiana na ugaidi la Umoja wa Mataifa UNCCT vyazindua mradi wa ubia dhidi ya ugaidi na imani kali kwa vijana

Mradi wazinduliwa kukabili itikadi kali na zenye ghasia

Amani na Usalama

Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa yamezindua mradi wa ubia wenye nia ya kukabiliana dhidi ya ugaidi ya ukereketwa wa kutumia mabavu.

Mradi huo unahusisha mbinu kadhaa ikiwemo kujengea uwezo vijana ili wajenge utamaduni wa amani usio na vurugu au ghasia.
 
Mkurugenzi mkuu wa shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa, UNESCO, Audrey Azoulay pamoja na Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na kukabiliana na ugaidi, Vladimir Voronkov wamezindua mradi kwa kuweka saini hati ya kuzindua mradi utakaowashirikisha pamoja  kuweza kuuendeleza.

Mradi wenyewe  utakuwa unaimarisha  kazi ya Umoja wa Mataifa ya kukabiliana na ugaidi na misimamo mikali yenye kusababisha vurugu, kupitia ushirikishi wa pamoja  na mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa kuweza kusaidia kutoa msaada mzuri kwa mataifa wanachama.
 
Mradi huo uliozinduliwa  mjini Paris Ufaransa unalenga kukabiliana na ukereketwa pamoja na ugaidi miongoni mwa vijana katika nchi za Morocco, Libya, Tunisia na Jordan kwa kuwawezesha vijana kufanya mambo ya maana kuliko ukereketwa.
 
Kuanzisha utamaduni wa amani na maendeleo endelevu ndio kitovu cha kazi za  UNESCO. 
 
Msisitizo  katika maendeleo endelevu kwa vijana ni mafunzo na utafiti, bila kusahau elimu kuhusu haki za binadamu, mbinu za uhusiano wa amani, utawala bora, kumbukumbu ya mauaji ya Holokosti, uzuiaji wa migogoro pamoja na ujenzi wa amani