Ingawa natoka kijijini, ubunifu umeniokoa- Lydia
"Baada ya kupata mafunzo ya usindikaji bidhaa, nimeona mafanikio makubwa sana katika kilimo na biashara na pia bidhaa zetu zinadumu muda mrefu bila kuharibika".
Hiyo ni kauli ya Lydia Jacob, mkulima na mjasiriamali kutoka Kisarawe, mkoa wa Pwani Tanzania.
Akihojiwa na Idhaa ya kiswahili ya Umoja wa Mataifa kando mwa mkutano wa kamisheni ya hali ya wanawake CSW62, jijini New York Marekani, Bi. Jacob amesema mafunzo ya usindikaji aliyopata yeye na wanawake wengine huko Kisarawe yamewasaidia katika kukuza kilimo na biashara ya korosho.
(Sauti ya Lydia Jacob)
Na kuhusu mafanikio aliyoyapata kwa kushiriki kutano wa kamisheni ya hali wa wanawake na pia kupata fursa ya kuonyesha biashara yake ambayo sasa imevuka mipaka ya Tanzania, Bi. Jacob anasema.
(Sauti ya Lydia Jacob)