Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kubadili maisha yako yahitaji kubadili mtazamo wako- Terry

Uwezeshaji wanawake na wasichana ndio muarobaini wa kufanikisha ajenda ya 2030. Pichanini Juba huko Sudan Kusini wanawake wakiwa kwenye maandamano.
UN /JC McIlwaine
Uwezeshaji wanawake na wasichana ndio muarobaini wa kufanikisha ajenda ya 2030. Pichanini Juba huko Sudan Kusini wanawake wakiwa kwenye maandamano.

Kubadili maisha yako yahitaji kubadili mtazamo wako- Terry

Wanawake

Mkutano wa 62 wa kamisheni ya hali ya wanawake, CSW62 uking'oa nanga hii leo, washiriki nao wanapaza sauti ni kipi wanafanya kubadili maisha ya wanawake wa vijijini. Leo tumezungumza na washiriki kutoka Monduli mkoani Arusha nchini Tanzania pamoja na kutoka kaunti ya Kwale huko Mombasa nchini  Kenya.

Washiriki wa mkutano wa 62 wa hali ya wanawake duniani wamezungumzia kile ambacho wanafanya mashinani ili kubadili maisha ya wanawake na wasichana wa vijijini, ikiwa ni katika kutekeleza azma ya hakuna anayeachwa nyuma. Assumpta Massoi na ripoti kamili.

(Taarifa ya Assumpta)

Nimepata fursa ya kuzungumza na baadhi ya washiriki akiwemo Terry Kunina, Afisa Programu wa shirika la kiraia la kukabiliana na ukatili dhidi ya wanawake, COVAW, ambaye amesema wanapatia wasichana wa kaunti ya Kwale huko Mombasa Kenya stadi za maisha ili wajiepushe na madhila kama vile biashara ya ngono lakini kuna changamoto.

(Sauti ya Terry Kunina)

Naye Maria Mamasita kutoka Monduli, mkoani Arusha nchini Tanzania akiwakilisha shirika la Naserian la kutetea haki za wajane amesema.

(Sauti ya Maria Mamasita)